Kwa nini fasihi ni sanaa?

                     FASIHI KWA UJUMLA
Dhana ya fasihi: Fasihi ni sanaa au ni tawi la sanaa linalotumia lugha katika kufikisha 
ujumbe wa msanii kwa hadhira iliyokusudiwa.
• Msanii ni nani? Msanii (fanani) ni mtu yeyote anayetunga kazi za kisanaa. 
• Hadhira ni nani? Hadhira ni wapokeaji wa kazi za kisanaa. Hadhira, wanaweza kuwa ni 
wasomaji au wasikilizaji/Watazamaji. 
SANAA
Sanaa ni uzuri unaojitokeza katika umbo lililosanifiwa na msanii. Mfano, uchoraji, 
uchongaji, ususi na kadhalika. 
AU
Ni ufundi wa kuwasilisha mawazo yaliyo katika fikra za binadamu. 
AINA ZA SANAA
Kuna aina tatu (3) za sanaa; 
(i) Sanaa za ghibu; ni aina ya sanaa ambayo uzuri wake hujitokeza kwa kusikiliza. Mfano, 
muziki, mashairi. 
(ii) Sanaa za maonesho; ni aina ya sanaa ambayo uzuri wake hujitokeza kwa kuona. 
Mfano, uchoraji, ususi, ufinyanzi. 
(iii) Sanaa za vitendo; ni sanaa ambayo uzuri wake hujitokeza kwa kuona na kusikiliza. 
Mfano, maigizo, tamthiliya. 

                 
Kutokana na maelezo hayo hapo juu, inadhihirisha kabisa kuwa fasihi ni tawi la sanaa na hasa ukiangalia katika mchoro wa sanaa, utakuta kuna kipengele cha fasihi ndani yake. 

Swali: Kwanini fasihi ni sanaa? 
Usanaa wa fasihi, unajidhihiriha katika mambo yafuatayo; 

1.Uteuzi mzuri wa lugha; 
 kwa kawaida kazi za fasihi, iwe fasihi simulizi au fasihi andishi huwa na lugha yenye 
ufundi, lugha hii huwavutia hadhira katika kuisikiliza au kuisoma kwake. Lugha ya 
kifasihi ni lugha iliyojaa matumizi ya methali, misemo, nahau na tamathali mbalimbali za 
semi na kadhalika. 

2.Mpangilio wa wahusika; 
Wasanii wa kazi za kisanaa hutumia ufundi wa kuwapanga wahusika ili wasaidie 
kufikisha ujumbe kwa hadhira zao. Wasanii huweza kuwachora wahusika halisi au 
wahusika wa kubuni na kuwapa majukumu yenye ufundi mkubwa kwa hadhira. 

3.Msuko wa visa na matukio; 
Maranyingi wasanii wa kazi za kifasihi hupanga matukio yao katika kazi zao kwa 
kutumia ufundi mkubwa. Wasanii wanaweza kupanga kazi zao moja kwa moja au 
kurukiana. Kitendo hiki hufanya baadhi ya wasomaji kuweza kuburudika zaidi pindi 
wanaposoma kazi hizo. 

4.Ubunifu; 
Mawazo aliyonayo msanii wa kazi za kifasihi yanatumia ubunifu mkubwa katika 
kuyawasilisha kwa hadhira. Mawazo hayo yanaweza kuibua furaha au huzuni kwa 
msomaji au msikilizaji. 

5.Uteuzi mzuri wa mandhari; 
Hata katika kuiteua mandhari katika kazi ya fasihi huhitaji ufundi. Wasanii huweza 
kutumia mandhari halisi au ya kubuni. Maranyingi, wasanii huchora mandhari, hata 
yakiwa ya kubuni lakini husadifu mandhari ya kawaida. Kitendo hicho hudhihirisha 
usanaa wa fasihi. 

Swali: Eleza tofauti kati ya fasihi na sanaa nyingine 
Ukiangalia katika mchoro wa sanaa, utaona kuna kipengele cha fasihi na sanaa nyinginezo 
kama vile; ususi, uchongaji, utarizi na kadhalika. Sasa swali la kujiuliza ni kwamba, sanaa 
hii ya fasihi inawezaje kutofautiana na sanaa nyinginezo? 
-Lugha;
 Ni kitu pekee kiachoweza kutofautisha kati ya fasihi na sanaa kama vile, uchongaji, ususi, 
ufinyazi na kadhalika. Ili iwe kazi ya fasihi ni lazima itumie lugha, iwe lugha ya 
mazungumzo au maandishi. Lakini sanaa kama uchongaji haitumii lugha katika kufikisha 
ujumbe wake kwa hadhira husika. 
- Utendaji
Kazi ya fasihi, huwa na utendaji yaani vitendo halisi hupatikana. Mfano, maigizo, miviga 
na kadhalika. Utendaji huu wa kazi za fasihi hushirikisha fanani na hadhira kwa wakati 
mmoja hasa katika fasihi simulizi. Tofauti na sanaa nyingine ambazo huwezi kuupata 
utendaji na ushirikishwaji wa fanani na hadhira kwa wakati mmoja. 

Kwa nini fasihi ni sanaa? Kwa nini fasihi ni sanaa? Reviewed by Machekoz.com on June 09, 2019 Rating: 5

12 comments:

FORM FOUR NECTA RESULT 2019

https://matokeo.necta.go.tz/csee/results/s5121.htm

Powered by Blogger.