Mwandishi ; Mwl GODLOVE J GWIVAHA
ENEO LA KAZI; SHULE YA SEKONDARYI TEGETA
MWAKA ;2015
1.Kwa kutumia mifano, thibitisha ubantu wa Kiswahili kwa hoja madhubuti (nect 2010 swali la 10)
KISWAHILI NI KIBANTU
Nadharia hii hutumia ushahidi wa kiisimu na kihistoria katika kuchunguza lugha ya Kiswahili katika mfumo mzima wa historia ya mgawanyiko wa kusambaa kwa lugha za kibantu. Nadhalia hii huitimisha kuwa Kiswahili ni mojawapo ya lugha katika jamii kubwa ya lugha ya wabantu.
Wataalamu wa nadharia hii ni kama vile makon Guthrie, meinhof c na rohlc.
Malcon Guthrie amethibitisha kuwa Kiswahili kilikuwepo kabla ya wageni na kimeonyesha kuwa Kiswahili kina uhusiano mkubwa na lugha za kibantu. Mwisho amehitimisha kwa kusema Kiswahili kimeanza Pwani ya afrika mashariki.
Mein holf na Rolh wao wanaamini kuwa wakati wa utawala wa washirazi katika upwa wa afrika mashariki kulikuwa na kabila la waswahili ambalo ni dhulia la wazaramo wa leo. Wazalamo walizaliwa katika harakati za biashara hivyo wakafuata nyayo za wazazi wao na lugha yao ilikuwa kibantu na kwa kuwa wabantu ni wengi zaidi lugha yao ikaanza kutumika na kuenea katika makabila mengine. Kutokana na waswahili kufanya biashara na waarabu, washirazi, wamalaysia, wahindi na wareno vifaa na majina ya vitu vya biashara vya wageni hao vikaenea na kuingizwa katika mfumo wa lugha hiyo ya kibantu.
Nadharsia hii imekubalika kuwa ndio sahihi juu ya asili ya Kiswahili kwa kuzingatia ushahidi wake wa kiisima na kihistoria.
USHAHIDI WA KIHISTORIA
Ushahidi wa kihistoria unathibitisha kuwa lugha ya kiswahili ilizungumzwakatika upwa au pwani ya afrika mashariki hata kabla ya ujio wa wageni kama vile waarabu, na wazungu.Ushahidi huu ulitolewa na wageni mbalimbali waliofika hapa afrika mashariki.wote wamehitimisha kwa kusema kuwa lugha ya Kiswahili ilizungumzwa hapa afrika mashariki hata kabla ya ujio wa wageni.
A.UGUNDUZI WA AL-IDRIS (1100-1166)
Ugunduzi huu ulifanyika huko sicily mnamo mwaka 1100-1166kwenye mahakama ya mfalme Roger , Al-idris alikuwa wa kwanza kugundua kuwa jina la kwanza la zamani la Zanzibar kuwa ni unguja. katika maelezo yake aliandika baadhi ya majina kama kikombe, mkono wa tembo,muriani na sukari ambayo ni majina ya ndizi mbalimbali zilizokuwa zikipatikana Zanzibar.
B.USHAHIDI WA MARCO POLO
Huyu ni mzungu ambaye alijishughulisha sana na maswala mbalimbali ya kijografia na alisafi sehemu nyingi duniani Marco polo aliandika hivi:
“Zanzibar ni kisiwa kizuri ambacho kina ukubwa na mzunguko wa maili 200. Watu wote wanaabudu (Mungu).Wana mfalme na wanatumia lugha yao, na hawalipi kodi (ushuru) kwa mtu.
Safari ya Marco polo
Aliandika kitabu cha kijografia ambacho kinasemekana kuwa hakikupata kuchapishwa lakini sehemu zake zimepatwa kufanisiwa kwa kirusi na kifaransa. Katika lugha ya Kiswahili ni kama ifuatavyo:
Katika visiwa vya Djawaga vilivyoshughulikiwa katika sura hii ni kile cha Andjaba ambacho mji wake mkuu unaitwa katika lugha ya kwao-zanzibar –ungudya na wakazi wake.
Japokuwa ni mchanganyiko kwa sasa wengi wao ni waislam chakula chao kikuu kikiwa ndizi, kuna aina tano ambazo zilijulikana kama kundi, fili ambao uzito wake waweza kuwa wakia 12, omani, mariyani, sukari.
Maelezo haya ya Marco polo yalithibitisha mambo ya msingi kuhusu wakazi wa pwani ya afrika mashariki na lugha yao.
C.USHAHIDI WA AL- MASUDI (915, BK)
Katika moja ya maandiko yake Al-masudi anazungumza juu ya wakazi wa mwambao ambao wanajulikana kwa jina la “Wazanji” kwa dhana hii neno Zanzibar linalotokana na neno “zanjibar” yaani pwani ya “Zenji” katika maelezo yake Al-masudi anaonyesha kuwa wazenji walikuwa na watawala, wakilimi ambao waliaminiwa kuwa walitawala kwa nguvu za Mungu.Kuna maelezo kuwa huanda neno wakilima lina maana ya wafalme.Al-masudi alisisitiza katika maelezo yake kuwa wazenji wasema lugha yao kwa ufasaha na walikuwa na viongozi waliohutubia kwa lugha yao, kutokana na neno Zenji kuna uwezekano kuwa kabla ya maajilio ya waarabu, Kiswahili kiliitwa “Kiazania” au Kizenji na wageni waliofika pwani ya afrika mashariki.
D. HISTORIA YA KILWA,Kimsingi habari zinaeleza historia ya kilwa karne 10-16 B.K na zinahusisha na kutajwa majina ya utani kama mkoma watu, nguo nyingi” nk ambao walipewa masltani wa kwanza wa kilwa Ali Ibnhussein na mwanae Mohamed Ibn Ali.Kutokana na habari hizi huenda lugha ya Kiswahili ilishaanzwa kusema mnamo karne ya 10 au ya 11 B.K. Maelezo juu ya sultani aliyeitwa Talt Ibn Al Hasani ambaye alipewa jina la utani “Hasha Hazifiki” nayo pia yalitolewa.
E.USHAIRI WA KISWAHILI
A. utenzi wa tambuka (karne ya 18 b.k)
Utenzi huuuliandikwa mnamo karne ya 18 kuanzia mwaka 1700 na kuendelea (tarehe kamili haijulikani). Utenzi huu umeandikwa kwa kutumia lugha (lahaja ya kimvita )ambayo ni moja ya lahaja za lugha ya Kiswahili.
B.Utenzi wa fumo liyongo
Shairi hili linasemekana liliandikwa karne 13 B.K. kuwepo kwa shairi hili kunadhihirisha uwepo wa lugha ya Kiswahili kabla ya hapo. Huenda kilianza kutumika kabla ya karne ya 10 B.K. baadhi ya beti za utenzi wa fumo liyongo ni hizi zifuatazo:
Ubeti 6 Liyongo kitamkali
Akabalighi vijali
Akawa mtu wa kweli
Na hiba huongeya
Ubeti 7 Kilimo kama mtukufu
Mpana sana mrefu
Majimboni yu maarufu
Watu huja kwangaliya
Ubeti 10 Sultani pate Bwana
Papo nne akanena
Wagala mumemwona
Liyongo kiwatokeya
Lgha hii ni mfano wa lugha iliyokuwa ikitumika mnamo karne ya 13 BK.ni wazi kuwa lugha hiyo ilianzwa kusemwa mapema kabla ya muda huo.
F.Vitabu vya peryplus na yu-yang-tsa-tsu,Kitabu cha perplus kinahusu mwongozo wa Bahari ya Hindi. Inasemekana kiliandikwa karne ya kwanza huko Alexandria.kitabu hiki kinataja habari za Tanzania (afrika mashariki) na habari za vyombo kama nyalawa, madema, mitepe. Kinaeleza kuwa watu wageni hutozwa ushuru na wafanyabiashara wenyeji, wanaijua pia lugha ya wenyeji wao.
Kitabu cha Yu-yang Tsa Tsu kinaeleza habari za upwa wa afrika mashariki na shughuli mbalimbali za wachina hapa afrika mashariki
Kitabu kingine kiliitwa Chu fan chi kilichochapishwa 1226 kinaelezea habari za Zanzibar na biashara, vyakula, dini, na wanyama wa pwani ya afrika mashariki.
G.Ushahidi wa ibn batuta karne ya 14 bk,Mohamed bin Abdallah Ibn Batuta ana asili ya taifa la kiarabu. Alikika upwa wa afrika mashariki mnamo mwaka 1331BK.katika maandishi yake anaeleza juu ya maisha ya watu wan chi hii ya afrika mashariki ingawa yeye aliita nchi ya waswahili. Anataja miji kama vile Mogadishu, na kilwa.anadai kuwa;
“Basi nilianza safari baharini kutoka Mogadishu kwend nchi ya ya waswahili na nchi ya kilwa ambao umo ndani ya nchi ya Zanji. Tulipofika Mombasa kisiwa kikubwa, mwendo wa siku mbili kutoka nchi ya waswahili…………….watu hawajishughulishi na kilimo, ingawa huagiza nafaka kutoka kwa waswahili”
Maelezo haya yanahusu eneo au mahali ambayo waswahili walikuwa wakiishi na inaonyesha kuwa watu hawa walikuwa wakiishi katika upwa au pwani wa afrika masharikikuanzia sehemu za bara upande wa kaskazini hadi msumbiji na bukini kwa upande wa kusini.
H.Maandishi ya Morice (karne ya 18 bk),Maandishi haya yalijitokeza mwaka 1776.katika maandishi yake morice amewagawa wakazi wa afrika mashariki katika makundi matatu yaani masuriyama,waarabu na Waafrika.Anaendelea kusisitiza kuwa Masuriyama na wafrika walisha kaa na kuungana kama jumuia moja wakaelewana na kusema lugha moja ya kisuriyama.Kuna wazo kuwa huenda kisuriyama ndicho Kiswahili cha leo.
USHAHIDI WA KIISIMU
Isimu ni nini?
Isimu ni sayansi au taaluma inayoiangalia lugha kwa undani(kisayansi) kwa kuzungukia tanzu kama vile;isimu jamii,isim historia,isimu linganishi,isimu matumizi,isimu nafsia na isimu fafanuzi.Ushahidi wa kiisimu ni ushahidiunaothibitisha kwa kutumia misingi inayohusu sayansi ya lugha.
Lugha ya Kiswahili ilifanyiwa utafiti na wataalamu kadhaa kwa lengo la kuainisha kama ina misingi ya kibantu.
Malcon Guthrie kutoka chuo kikuu London Uingereza alitumia miaka 20 kuchunguza uhusiano uliopo baina ya lugha za kibantu ziliko katika eneo lote ambalo hukaliwa na wabantu yaani kusini mwa jangwa la sahara.
Alifanya Uchanganuzi wa mashina au mzizi(viini) ya maneno 22000 kutoka lugha 200 za kibantu .Kibantu Uchunguzi wake alikuta mzizi (mashina)2300 imezagaa katika lugha mbalilmbali za kibantu na kiswahli kikiwezo.Mashina au mizizi 500 yalilingana katika lugha zote 200.Mashina haya yalipatikana katika lugha zote za kibantu.Mashina haya yalikuwa ya asili moja.Baadhi ya lugha hizo 200 zilizofanyiwa uchunguzi,lugha ya Kiswahili ilionesha kuwa na ulinganifu sawa na kikongo(44 asilimia)
Katika kuchunguza ni asilimia ngapi za mashina hayo 500 yamo katika kila lugha ilionekana mgawa ufuatao;
Kiwemba kizunguzwacho Zambia 54%
Kiluba kizungumzwacho Katanga 51%
Kikongo kizungumzwacho 44%
Kiswahili kizungumzwacho Afrika Mashariki 44%
Kisukuma kizungumzwacho Tanzania 41%
Kiyao kizungumzwacho Tanzania/Msumbiji 35%
Sotho kizungumzwacho Botwana 20%
Rundi kizungumzwacho Burundi 43%
Kinyoro kizungumzwacho Uganda 37%
Zulu kizungumzwacho Afrika kusini 29%
Matokeo ya utafiti huu yanathibitisha kuwa;
i. Mashina mengi ya lugha za kibantu yapo afrika ya kati hasa sehemu zinazozungumkia mkoa wa Katanga huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kupungua kadri unavyoelekea mbali nako. Hivyo ni dhahiri kuwa wabantu walienea kutoka sehemu hizo na kuja sehemu mbalimbali zikiwemo zile za afrika mashariki.
ii. Kufuatana na matokeo ya utafiti hua ni wazi kuwa, lugha ya Kiswahili ni kibantu kama madai yake ya kusema Kiswahili madai yake ni kiarabu yangekua sahihi basi lugha hiyo ingehusiana mno na kiarabu.
1. MSAMIATI,Msamiati ni msingi wa lugha ya Kiswahili na kibantu unafanana kabisa. Msamiati wa msingi ni ule unaohusu ambayo hayabadiliki badiliki kutokana na mabadiliko ya utamaduni tofauti zinaweza kujitokeza katika matamshi au mabadiliko kidogo ya viambishi, kakini si katika mzizi.
Mfano;
Kiswahili kindali kizigua kijita kikurya
Mtu umundu mritu omontu omonto
Maji amishi manzi amanji amanche
Moto umlilo moto omulilo omoro
2. Tungo (sentensi) za Kiswahili ,miundo ya tungo (sentensi) za maneno ya Kiswahili zinafanana sana miundo ya tungo za maneno ya kibantu. Sentensi za kiswahili na lugha za kibantu zina kiima na kiarifu.
Mfano Kiswahili – Juma/ anakula ugali
K A
Kizigua – Juma/ adya ugali
K A
Kisukuma – Juma/ alelya bugali
K A
Kindali – Juma /akulya ubhugli
K A
Kijita –Juma/ kaiya ubusima.
K A
3.Ngeli za majina,Hapo kuna makubaliano kufuatana na ngeli katika mambo ya nomino (umoja na wingi wa majina) pamoja na kisarufi.
i. Kigezo cha maumbo ya majina
Kigezo hiki hufuata mambo ya umoja na wingi katika kuyaainisha majina. Majina yaliyo mengi katika lugha ya Kiswahili na lugha za kibantu hufuata mkondo wa umoja na wingi. Majina ya lugha ya Kiswahili na lugha za kibantu yaliyomengi yana maumbo dhahiri ya umoja na wingi.
Mfano Umoja wingi
Kiswahili Mtu Watu
Mtoto Watoto
Kikurya Omonto Banto(abanto)
Omona Baria (abana)
Kizigua Mntu Bhantu
Mwana Bhana
Kindali Mundu Bhandu
Mwana Bhana
ii. Kigezo cha upatanisho wa kisarufi
Katika kigezo hiki tunaangalia uhusiano uliopo kati ya nomino na kivumishi na viambishi vya awali vya nafsi katika vitenzi vya Kiswahili na kibantu.vivumishi majina pamoja na vitenzi hivyo hubadilika kutokana na maumbo ya umoja na wingi.
Mfano
Umoja wingi
Kiswahili Baba analima Baba wanalima
Kindali Utata akulim Abhatata Bhakulima
Kikury Tata anarema Batata abalima
Kijita Tata kalmia Batata abalima
3. Vitenzi vya kiswahili na kibantu,Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya vitenzi vya Kiswahili na vile vya kibantu. Vipengele vinavyothibitisha uhusiano huu ni viambishi, mnyambuliko pamoja na mwanzo/mwisho wa vitenzi.
a. Viambishi
Lugha ya Kiswahili na lugha za kibantu vitenzi vyake hujengwa na mzizi (kiima) pamoja na viambishi vyake (awali na tamati)
Mfano
Kiswahil – analima – a-na-lim-a
1 2 3 4
Kikurya – ararema – a-ra-rem-a
1 2 3 4
Kindali- akulima – a – ku – li – ma
1 2 3 4
ü Kiambishi awali kipatanishi cha nafsi.
ü Kiambishi awali cha njeo.(wakati uliopo)
ü Mzizi /kiima
ü Kiambishi tamati
b. Mnyambuliko wa kitenzi (uambishaji)
Mnyambuliko ni kitendo cha kuunda neno jipya kwa kuunganisha viambishi kwenye mzizi wa shina au neno mnyambuliko wa vitenzi vya Kiswahili hufanana na ule wa vitenzi vya lugha ya kibantu.
Mfano
Kiswahili – kucheka – kuchekesha – kuchekelea
Kindali – kuseka – kusekasha – kusekelela
Kibena – kuheka – kuhekesha – kuhekelela
Kinyamwezi – kuseka – kusekasha – kusekelela
Kikagulu – kuseka – kusekesha – kusekelela
c. Mwanzo wa vitenzi
Vitenzi vyote vya Kiswahili na vile vya lugha za kibantu huanza na viambishi ambavyo ni viwakilishi vya nafsi:
Mfano
Kiswahili - Ninakwenda
Kihaya – Ningenda
Kiyao - Ngwenda
d. Mwisho wa kitenzi
Vitenzi vya lugha za kibantu huishia na Irabu a
Mfano
Kiswahili – kukimbia – kuwinda – kushuka.
Kindali - kukinda – kubhinga – kukola
Kisukuma - kwihuka -
Jinsi ya kujibu maswali ya historia ya lugha
Reviewed by Machekoz.com
on
December 29, 2018
Rating:
No comments: